Wednesday, 21 March 2012

MECHI ZA 21 MARCH 2012 - LIGI KUU YA UINGEREZA

22:45 Manchester City 2-1 Chelsea
22:45 Tottenham 1-1 Stoke
23:00 Everton 0-1 Arsenal
23:00 QPR 3-2 Liverpool

NB Saa za Afrika Mashariki

Man City point 1 uani kwa Man Utd!  Tevez atoa pande kwa Nasri na kupata bao.
Chelsea ya endelaza mduara , kunyume nyume....!
Tottenham yatoa zawadi kwa Arsenal kujongea nafasi ya 3!
Arsenal wajongea nafasi ya 3!
Liverpool wadondosha point 3 muhimu dk za majeruhi!

Msimamo wa Top 5 baada ya mechi (point mabanoni)-1.Man Utd (70), 2.Man City (69), 3.Arsenal (55), 4.Tottenham (54), 5.Chelsea (49)


------------------------------------------------------------------------------------------------------
Big news: kurudi kwa Tevez! Baada ya kuingia mitini tangu Sept 2011 kufuatia mzozo kati yake na Manager wake,Mancini. Tevez uenda akachezeshwa kwenye mechi hii. Tevez aliahidi kutochezea tena Man City chini ya Mancini, wakati Manager wake alisema ni ndoto kwa Tevez kurudi Man City. Je washabiki watamzomea ama watamshangilia?

Man City ipo nafasi ya 2 na point 66, point 4 nyuma ya vinara wa ligi Man Utd aka mashetwani Wekundu.

Chelsea yenye point 49 ipo nafasi ya 5, nyuma ya Arsenal kwa tofauti ya point 2. Hii ni nafasi ya kuchukua nafasi ya 4 kama Arsenal watapoteza mechi yao.  

Tottenham iliyopo nafasi ya 3 na point zake 53, mmhh point 1 mbele ya Arsenal! Wachezaji wa Tottenham labda bado wanayo shock ya mechi iliyopita ya FA kati yao na Bolton, uenda Stoke wakatumia upenyo huo.

Everton waliwapiga Tottenham 1-0 kwenye mechi ya 10 March, Feb 11 waliwapiga Chelsea 2-0 Feb ingawa walipigwa na Liverpool 3-0  mechi ya March 13. Sasa ni wakati wa kuidhalilisha Arsenal. 

Arsenal wameshinda mechi zao tano za ligi kuu zilizopita, wanazo point 52 katika nafasi ya 4. Kuna hatari ya Arsenal kuchukua nafasi ya 3 kama Tottenham wasiposhinda mechi yao.

Msimamo wa Top 5 kabla ya mechi -
1.Man Utd (70), 2.Man City (66), 3.Tottenham (53), 4.Arsenal (52) 5.Chelsea (49)

No comments:

Post a Comment