15:45 Bolton 2-1 QPR
18:00 Aston Villa 1-0 Fulham
18:00 Chelsea 1-0 Stoke
18:00 Sunderland 1-0 Liverpool
18:00 Wolves 0-2 Blackburn
20:30 Everton 1-0 Tottenham
NB: Saa za Afrika Mashariki
Mhhhh! Bwawa la maini (liverpool), nini tena, jahazi linazama ama ndio style mpya ?
Chelsea ushindi mkononi imefikisha point 49 sawa na Arsenal, na kumsukuma Arsenal nafasi ya 5, haya Gooners kazi ipo Jumatatu kurudi nafasi ya 4.
Tottenham kama kawa kizunguzungu kinatawala, ule mchezo wa kurudi kinyume nyume ahhh, si haba! Imekwama na point zake 53 ,Chelsea na Arsenal hao wanapumulia mgongoni!
---------------------------------------------------------------------------------------------------
Kabla ya mechi
Chelsea inazo point 46 ipo nafasi 5, nyuma ya Arsenal kwa point 3. Ushindi wa point tatu na magoli zaidi ya 2 utaisogeza nafasi ya 4. Nayo Stoke iliyopo nafasi ya 9 na point 36, itafanya kila jitihada kupata point kujiimarisha kwenye top 10.
Liverpool ipo nafasi ya 7 ina point 39, ipo hatarini kushuka mpaka nje ya top 10. Ushindi ni muhimu kujizatiti kwenye nafasi ya 7 huku wakijiandaa kucheza mechi nyingine Jumanne dhidi ya Everton. Sunderland nao wakishinda watajitoa kwenye nafasi ya 12 na kuingia nafasi kati ya 10 mpk 8.
Tottenham ipo nafasi ya 3 kwa point 53, kazi wanayo kujikita vizuri kwenye nafasi ya 3, ambayo muda sio mrefu uenda ikachukuliwa na Arsenal inayocheza Jumatatu yenye point 49 a.k.a mechi 1 na ushee! Everton ni wagumu na wanachezea uwanja nyumbani, watafanya kila jitihada kujitoa nafasi ya 13, ushindi unaweza kuwasogeza nafasi kati ya 8 hadi 10.
Mechi za kesho: 17:00 Man Utd v West Brom, 17:00 Swansea v Man City, 19:00 Norwich v Wigan
Top 10 ilivyokuwa kabla ya mechi za leo (point mabanoni):-
1.Man City (66), 2.Man Utd (64), 3.Tottenham (53), 4.Arsenal (49), 5.Chelsea (46), 6.Newcastle (44), 7.Liverpool (39), 8.Fulham (36), 9.Stoke (36), 10.West Brom (35)
No comments:
Post a Comment