Saturday 14 January 2012

AINA MPYA YA NYOKA, ANAPATIKANA TANZANIA TU - MATILDA'S HORNED VIPER

Snake picture: Matilda's horned viper closeup
Matilda

Nyoka huyu anaitwa Matilda, ni wa aina ya pekee duniani na anapatikana kusini mwa Tanzania tu!

Aligunduliwa miaka miwili iliyopita (2010-2011), na mwezi uliopita aliidhinishwa rasmi kama aina mpya ya nyoka duniani.

Matilda anayo magamba ya rangi ya njano na nyeusi, macho ya kijani, urefu wa zaidi ya 2ft, na magamba yaliyojitokeza mfano wa pembe mbili.

Jina la nyoka Matilda limetoka kwa mtoto anayeitwa Matilda (aliyekuwa na miaka mitano) aliyevutiwa na kupenda kumwangalia nyoka huyo.  Mtoto huyo ni wa Mwanasayansi / Director wa Wildlife Conservation Society ( Tanzania), Mr Tim Davenport aliyeongoza utafiti wa nyoka huyo.

Eneo halisi analopatikana nyoka hao alijatajwa, ili kudhibiti maharamia.

For more-  http://news.nationalgeographic.com/news/2011/12/pictures/111230-snakes-horned-vipers-tanzania-secret-animals-science/#/new-species-matildas-horned-viper-face_46392_600x450.jpg


No comments:

Post a Comment