Friday 2 December 2011

UCHAGUZI USA- MGOMBEA WA REPUBLICAN MATATANI

Mmarekani mweusi, Herman Cain anaye gombea ticket ya kugombea urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani amekiri kuwa na mahusiano nje ya ndoa (aka nyumba ndogo) kwa miaka 13.

Cain ambaye alikuja kwa kasi kubwa na alitarajiwa na wengi kujishindia nafasi ya hiyo ili kupambana na Baraka Obama (Democratic)  kwenye kinyang'anyiro cha kugombea urais November 2012, amekumbwa na mfululizo wa kashfa za mausiano na wanawake wapatao watano mpaka sasa.

Kashfa inayorindima kwa sasa ina muhusisha Cain na mwanamke anayeitwa Ginger White, amekiri kumpatia mwanamke huyo fedha za matumizi. Pia inasemekana amekuwa akiwasiliana na mwanamke huyo kwa njia ya ujumbe wa simu (sms) si chini ya mara 70 kati ya October na November 2011. Na amekiri kwamba ajamfahamisha mke wake kuhusu uhusiano huo.


Cain amedai amekuwa akiwasaidia wengi wenye shida, na ajawahi kukutana kimwili na Ginger White. Amesema anatarajia kujua hatma ya campaign zake atakapo onana  na mke wake (Mrs Cain) leo. (http://www.bbc.co.uk/news/world-us-canada-15996701)


Unadhani nini kitatokea? Kujitoa kwenye kinyang'anyiro.

No comments:

Post a Comment