Sunday 9 October 2011

VETEL ACHUKUA UBINGWA WA Fomula 1 2011

Kama ilivyotarajiwa, Vetel amechukua Ubingwa wa Fomula 1 kwa msimu wa 2011.

Kwa mafanikio hayo ameweka record (historia) ya kuwa dereva mwenye mdogo kati ya waliofanikiwa kuchukua ubingwa kwa miaka miwili mfululizo, kwani amekuwa bingwa kwa misimu miwili ya 2010 na 2011.

Katika race hizo za Japan Grand Prix (Suzuka), Vetel alimaliza katika nafasi ya nne na kujipatia point 15, hivo kuwa na jumla ya point 324 takea msimu uanze na ambazo azitaweza kufikiwa na dereva mwingine yeyote msimu huu, huku kukiwa kumesalia 4 races kumalizia msimu.

Kwa upande mwingine ule mzimu unaomsakama Hamilton umeendelea katika race hizo za Japan, kwa mara nyingine alikwaruza gari la Massa (  http://www.youtube.com/watch?v=fjwXyEwdRNk ), lakini Hamilton aliponea bila kupewa adhabu yoyote. Hata hivo uenda Massa hatachukulia kitendo hicho kirahisi tusubiri nini kitatokea race zinazofuata!

Button alishinda race hizo akifuatiwa na Alonso, kama ifuatavyo (top seven):-

   Driver           Point          Jumla  ya Point kwa msimu                       
1. Button                25                                210
 2.Alonso               18                                202
3. Vetel                  15                                324
4. Webber             12                                194
5. Hamilton            10                               178
6. Schumacher      8                                  60
7. Massa                 6                                 90

Kwa matokeo hayo msimamo tangu msimu kuanza ni :- 1.Vetel (324),  2. Button (210), 3. Alonso(202), 4.Webber (194) 5. Hamilton (178), 6. Massa (90)

Race zinazofuata ni za Korean Grand Prix weekend ijayo tarehe 14 -16 October, hivo takae mkao kushuhudia yatakayojiri.


No comments:

Post a Comment