Friday 19 August 2011

MKURUGENZI WANYAMA PORI ASIMAMISHWA KAZI

Sakata la tuhuma za ufisadi wizara ya Maliasili na Utalii, limechukua sura mpya kwani Mkurugenzi wa Wanyama Pori  Obeid Mbagwa na maofisa wengine wawili, wamepewa likizo ya lazima ili kuruhusu uchunguzi kufanyika

Hatua hizo zimechukuliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mh Maige ,baada ya jana Waziri mkuu Pinda alipositisha usafirishaji wa wanyama  pori nje ya nchi kwa mwaka mmoja.

Hatua zote hizo zimechukuliwa kufuatia tuhuma zilizotolewa bungeni kuhusu usafirishaji wa wanyama pori uliofanyika kinyemela kupitia uwanja wa ndege wa KIA tarehe 24/11/2010 kwa ndege iliyosajiliwa Qatar.

Wizara hii imeshutumiwa mambo mengi ikiwemo kuwa na Ukabila (Wabena) tetesi zilimgusa Luhanjo ingawa amekanusha, na utoaji vibali 180 vya uwindaji katika kipindi kifupi swala hili linamgusa Mbanga.

for more- http://www.mwananchi.co.tz/component/content/article/37-tanzania-top-news-story/14639-vigogo-watatu-wasimamishwa-kazi-kashfa-ya-wanyamapori.html

No comments:

Post a Comment