Katika kile kilichotegemewa na wengi, Mr Sugu alitumia nafasi na wadhifa wake vizuri bungeni tarehe 11/08/11 kuelezea vilio na malalamiko ya wasanii wengi nchini.
Baadhi ya yale aliyogusia ni:-
-Udhibiti wa vyombo vya habari vya serikali
Mfano aliitaka serikali kueleza ni hatua gani zilichukuliwa dhidi ya muhariri mkuu wa gazeti la Daily News kama inavyofanya kwa vyombo vingine vya habari,kuhusu Article iliyotolewa wakati wa uchaguzi iliyosema ' Kamwe Dk Silaa hatashinda uchaguzi'
-Haki ya kupata habari na Huduma ya vyombo vya habari:
Serikali ifikishe mapendekezo ya wadau wa sanaa bungeni kuhusu sheria hizo ili yapitishwe kuwa sheria, na ameonya serikali kutochakachua maoni hayo.
-Benki ya vijana:
Benki hiyo ianzishwe ili iweze kuchochea ajira kwa vijana.
-Baraza la vijana la taifa lianzishwe
-Mabadiliko uongozi idara ya vijana
-Uimarishaji wa sekta ya utamaduni
-Udhibiti wa mapato ya sekta ya sanaa:
ili kuchangia kodi serikalini, mfano alisema ni 12% tu ya shughuli za wasanii zinatozwa kodi wakati 87% azitozwi. Hivo amesisitiza COSOTA ibadilishwe na kuwa CORATA.
Na amesisitiza udhibiti wa mapato ya wasanii kutoka nje wanapokuja kufanya maonyesho nchini, ili watozwe kodi ipasavyo.
Studio ya JK iliyotolewa kwa wasanii pamoja na Jengo:
Amebainisha kwamba Studio na Jengo la serikali kwaajili ya studio hiyo vimechukuliwa na NGO binafsi yaani THT, na ametaka serikali kuhakikisha studio na jengo hilo kukabidhiwa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).
Nyumba ya sanaa:
Ameitaka serikali kurudisha Nyumba ya sanaa serikalini
Kufuatilia mapato yote yaliyoingizwa na board hiyo iliyofutwa mwaka 2005
Pia aliikumbusha serikali kurejesha viwanja vilivyochukuliwa na CCM virejeshwe chni ya serikali kwa faida ya Watanzania wote, alitaja viwanja vifuatavyo: Kirumba (Mwanza), Sheik Amri Abeid (Arusha),Majimaji (Songea) na viwanja vya Dodoma na Songea.
pata sehemu ya hotuba hiyo- http://www.youtube.com/watch?v=qrIOa_JuAnA
No comments:
Post a Comment