Tuesday 9 August 2011

MAUZO YA UDA ,MAFISADI WAHUSISHWA!

Kasheshe la shirika la UDA ni ufisadi mtupu.

UDA imebinafsishwa kinyemela, na waziri mkuu kwa niaba ya serikali ameamrisha uchunguzi ufanywe na kamati ya bunge ya miundo mbinu, cha kushangaza kwenye kamati hiyo kuna kigogo  (Prof Kapuya) ambaye ni mmiliki wa share kwenye shirika la Simons Group lililonunua UDA

Spika wa bunge naye ameteua kamati ya POAC iliyopo chini ya Mh.Zitto  kufanya uchunguzi baada ya kujua kungekuwepo confict of interest katika uchunguzi ambao ungefanywa na kamati hapo juu.

Kwa ufupi shirika la Usafiri Dar es salaam (UDA) inasemekana liliuzwa kinyemela, lkn tuhuma zimeibua ufisadi kufanyika, ambapo malipo ya mauzo ya shirika hilo ($200,000 kati ya $1m) yaliingizwa kwenye a/c binafsi ya aliyekuwa mwenyekiti wa shirika la UDA(Iddi Simba) ambaye aliwahi kuwa waziri kwenye serikali zilizopita, ingawa amekanusha kwamba malipo hayo ayana uhuziano na mauzo hayo.

for more
- http://www.mwananchi.co.tz/component/content/article/37-tanzania-top-news-story/14342-spika-amtwisha-zitto-kabwe-zigo-la-uda.html

- http://allafrica.com/stories/201108081936.html

- http://allafrica.com/stories/201108070099.html

No comments:

Post a Comment