Bw Mabere Marando ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, ametaja majina ya watu wanaousishwa na kesi inayo mkabili Mkurugenzi wa ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Lwakatare.
Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari, Bw Marando amesema atajiunga katika jopo la wanasheria kumtetea Lwakatare kwasababu uchunguzi umeonyesha kwamba kesi hiyo ni ya kisiasa na sio ya kisheria kama alivyodhani awali.
Taarifa hiyo imehusisha majina ya watu kadhaa wanaotuhumiwa kuhusika na mpango wa kumteka Kibanda. Baadhi ya watajwa ni pamoja na Nchemba, Ridhiwani, n.k, ambao Mabere amesema mawasiliano kati yao yalifanyika ili kufanikisha utekaji na utesaji wa Kibanda.
Pia orodha yake imemuhusisha Muhidini Michuzi kutokana na ujumbe wake wa barua pepe (email) aliyotuma kwenda kwa ofisi ya Rais ya Binafsi (OBR) na Usalama wa Taifa (TISS) kupongeza TISS kufanikisha kupatikana video ya Lwakatare.
Bw Mabere Marando amesema ataiomba mahakama kutoa rekodi za mawasiliano ya simu za watajwa hao.
Kujua zaidi twanga link - http://www.youtube.com/watch?v=SjZkNKkHAcs ama http://chademablog.blogspot.co.uk/2013/04/chadema-yawataja-10-utekaji-kibanda.html#more
No comments:
Post a Comment