Saturday, 9 March 2013

RAILA KUPINGA MATOKEO MAHAKAMANI, UHURU AWASHUKURU WAPIGA KURA

Baada ya mshindi wa urais nchini Kenya kutangazwa na tume (IECB), Uhuru Kenyatta na Raila Odinga wametoa kauli zao.

Raila Odinga ambaye ni mgombea wa muungano wa CORD ameeleza kutoridhishwa na matokeo sababu ya hitilafu zilizojitokeza kwenye zoezi zima la upigaji na kuhesabu kura. Raila amethibitisha kwamba atapeleka madai yake kortini ili kupata ufumbuzi na kuwataka wananchi kuwa watulivu...

Uhuru Kenyatta wa Jubillee Alliance aliyeshinda uchaguzi huo, amewashukuru wapiga kura kwa ushirikiano wao na kuahidi kwamba atatekeleza ahadi zake. Pia amewataka wananchi kuendelea na shughuli za kujenga taifa..

No comments:

Post a Comment