Saturday, 9 March 2013

UHURU KENYATTA ASHINDA UCHAGUZI MKUU WA KENYA, IECB YATHIBITISHA

Tume inayosimamia uchaguzi nchini Kenya (IECB) imemtangaza mgombea urais wa Jubilee Alliance, Uhuru Kenyatta kama mshindi  wa uchaguzi uliofanyika 4 March 2013.
 
Mwenyekiti wa IECB, Bw Issack Hassan alisema Uhuru alipata jumla ya kura 6,173,433 ikiwa ni 50.07%. Idadi hiyo imezidi kwa jumla ya kura 832,887 ya idadi alizopata Raila  ambazo ni kura 5,340,546 na jumla ya kura zilizopigwa ilikuwa 12,330,028 ( https://www.youtube.com/watch?v=vtKXZ-oFlI4&feature=player_embedded )
 
Kwa mujibu wa taratibu mshindi nafasi ya rais alitakiwa kupata angalau 50% ya kura zote. Pia angalau 25% ya Counties 47, idadi ambayo Uhuru na Odinga walifanikiwa kufikisha. 
 
Hata hivyo Raila anatarajiwa kupinga matokeo hayo mahakamani kwa madai ya kuwepo uchakachuaji.
 
Ni mara ya tatu Raila kugombea nafasi ya rais. Aligombea 1997 dhidi ya Daniel A Moi na Mwai Kibaki ambapo Moi alishinda. Kwenye uchaguzi mkuu wa 2002 Raila akugombea na badala yake alimuunga mkono Kibaki ambaye alishinda.

Kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2007, Raila aligombea nafasi ya rais dhidi ya Mwai Kibaki,  alishindwa na kugomea matokeo. Kulizuka machafuko yaliyo sababisha vifo vya watu zaidi ya 1000. Baada muafaka kupatikana wa kuundwa kwa serikali ya mseto ambapo Kibaki alishika nafasi ya rais na Raila alipewa nafasi ya Waziri mkuu. Naibu wake alikuwa ni Uhuru.

Kushinda kwa uhuru umetimiza miaka 50 tangu baba yake, Jomo Kenyetta alipoingia madarakani mwaka 1963 kama Waziri mkuu wa kwanza wa Kenya.


Kushoto ni rais mteule Uhuru na kulia ni Ruto makamu wake
 
Uhuru Kenyatta na William Ruto wanakabiliwa na mashtaka kwenye Mahakama ya Kimataifa (ICC: Internatinal Criminal Court) kuhusiana na machafuko yaliyo tokea baada ya uchaguzi mkuu wa 2007.
 

No comments:

Post a Comment