Baada ya Spika kutupilia mbali hoja ya Mh Mnyika iliyomtaka Waziri wa Maji, Professor Jumanne Maghembe kutoa majibu ya tatizo la maji Dar es Salaam, imewagharimu CCM kwenda kutoa jibu kwa wananchi kama walivyo amrishwa na Mh Mnyika.
Terehe 10 Feb 2013 CHADEMA ilifanya mkutano kwenye viwanja vya Temeke Mwisho jijini Dar es Salaam, ambapo Mh Mnyika alimpa waziri wa Maji wiki mbili kutoa majibu kuhusu hoja tisa zikiwemo za: ufisadi wa billioni Ths240 za bomba la Wachina, Ufisadi wa billioni Ths96 za usambazaji wa maji nchi nzima, na tatizo la maji taka na safi Dar es Salaam, la sivyo maandamano yafanyike kumshinikiza waziri huyo kutoa majibu.
Mh Mnyika kwenye mkutano wa Temeke, 10 Feb 2013
15 Feb 2013, Mh Mnyika alitoa ufafanuzi kuhusu ufuaitiliaji wake wa DAWASA na DAWASO, na alimkumbusha waziri wa Prof. Maghambe kutoa majibu ili kuepusha maandamano.( http://chademablog.blogspot.co.uk/2013/02/taarifa-ya-hali-ya-upatikanaji-wa-maji.html)
Jumamosi ya 16 Feb 2013, ikiwa ni wiki moja tu, CCM imefanya mkutano kwenye viwanja hivyo vya Temeke Mwisho ambapo Waziri wa Maji, Professor Jumanne Maghembe ametekeleza amri ya Mh Mnyika kwa kutoa jibu kuhusu tatizo la maji, kwa ahadi ifuatayo,
“Serikali imejianda kuhakikisha kwamba Mkoa wa Dar es Salaam unakuwa na maji ya kutosha katika mpango wake wa muda mfupi na mrefu. Katika mpango wa muda mfupi mpaka kufikia Aprili 2014, maji yatakuwa ya kutosha katika jiji hili,”
Pia amesema kwamba serikali ina mpango wa kutandaza mabomba ya maji kutoka Ruvu Juu mpaka Dar es Salaam kupitia Bagamoyo, na uchimbaji wa visima 84.
Tatizo la maji Dar litaisha April 2014 ?Mh Mnyika ataridhika na ma jibu hilo? Ufuatiliaji ni muhimu.....
Tatizo la maji Dar litaisha April 2014 ?Mh Mnyika ataridhika na ma jibu hilo? Ufuatiliaji ni muhimu.....
No comments:
Post a Comment