Sunday, 24 June 2012

NDEGE YA RAIS WA MALAWI IKIUZWA, YA TANZANIA JE?

Viongozi wa Afrika wanaishi maisha ya kifahari, tofauti na maisha ya walipa kodi.

Mwezi  May rais wa Malawi, Joyce Banda alitangaza nia ya kutaka kuuza ndege ya rais na magari ya kifahari ya serikali, nakudai yupo tayari kupanda ndege za kukodisha.

Mwaka 2009, serikali ya marehemu Rais Mutharika ilinunua ndege aina ya Jet- Dassault Falcon 900 EX, iliyo tengenezwa nchini France. Ndege hiyo ilikadiriwa kugharimu dola za Kimarekani milioni 22.4, na ilikadiriwa kugharimu ya dola laki 3 za Kamarekani kila mwaka.

Rais Joyce Banda tangu akabidhiwe madaraka baada ya kifo cha Mutharika, amefanya mabadiliko mengi ya kiuchumi ili kuinusuru Malawi kutoka kwenye janga la kiuchumi.

Uenda ndege ya serikali ya Tanzania aina tofauti na ile ya Malawi. Hata uchumi wa Tanzania hauna tofautiani na Malawi.

Riporti ya Umoja wa Mataifa (UN Human Dev Index Trend 2008-2011) inaonyesha kimaendeleo duniani, Tanzania ni ya 152, na Malawi ni ya 171. Kwa wastani wananchi wenye kipato chini ya dola 1.25 za Kimarekani kwa siku, Tanzania ni 67.9% , na malawi ni 73.9% (UN Human Development Report 2009).

Budget ya mwaka 2012/13 inaonyesha kwamba Tanzania bado inategemea misaada na mikopo kutoka nje ya nchi.

Iweje wananchi wanakosa huduma muhimu wakati viongozi wanaishi maisha ya kifahari? Wabunge wetu wamefanyia nini swala la gharama ya ndege na magari ya serikali?

No comments:

Post a Comment