Sunday, 24 June 2012

FERNANDO ALONSO ASHINDA EUROPEAN GRAND PRIX

Ingawa alianza akiwa nafasi ya 11 kwenye race za European Grand Prix zenye mizunguko (laps) 57, Fernando Alonso (Ferrari) ameibuka na ushindi.

Vetel (Redbull) aliyenza katika nafasi ya kwanza alijikuta akishindwa kuendelea na race hizo baada ya gari lake kupata itilafu kwenye mzunguko wa 36.

Hamilton (McLaren) naye ingawa alianza katika nafasi ya pili, katika mzunguko wa 55 alipoteza nafasi hiyo ikachukuliwa na mkongwe Raikkonen (Lotus).

Ikiwa imebakia mizunguko miwili kufikia mwisho (mzunguko wa 56), Hamilton na Maldonaldo (Williams) waligongana na matokeo yake wakashindwa kuendelea, hivyo kutoa zawadi ya nafasi ya tatu kwa mkongwe Michael Schumacher (Mercedes).

Tangu mwanzo wa msimu, msimamo wa Top 8 (point kwenye mabano) nikama ifuatavyo:

1. F.Alonso (111), 2.M.Weber (91), 3.L Hamilton (88), 4.S Vetel(85), 5.N Rosberg (75), 6.K Raikkonen (73), 7.Grosjean (53), 8.J Button (49)

Race zinazofuata 8 July 2012: British Grand Prix, Silverstone

No comments:

Post a Comment