Tuesday, 19 June 2012

Mh MNYIKA AFUKUZWA KWENYE KIKAO CHA BUNGE !

Mh John Mnyika alionyeshwa mlango wa kutoka nje ya kikao cha bunge baada ya  kukataa kufuta kauli yake.


   Mh Myika akipiga misele baada ya kutoka kikaoni

Amri ya kutolewa nje ya kikao ilitolewa na naibu wa spika, John Ndungai baada ya Mh. Myika kutamka ifuatavyo....

tumefika hapa tulipo kwa sababu ya udhaifu wa Rais Kikwete, tumefika hapa tulipo kwa sababu ya uzembe wa wabunge na bunge, na tumefika hapa tulipo kwa sababu ya upuuzi wa CCM'

Mh Mnyika alidai kwamba ubovu wa budget iliyosomwa, na sababu za kushindwa kutekelezwa kwa mipango ya budget iliyopita unatokana na udaifu wa taasisi ya rais.

Akitetea kauli baada ya kuondolewa kwenye kikao, Mh Mnyika alisisitiza kwamba rais pekee ndiye mwenye mamlaka ya kuiondoa budget, sababu wabunge wakikataa budget, bunge litavunjwa!



Chimbua humu -  http://mnyika.blogspot.co.uk/2012/06/msimamo-wangu-wa-sasa-juu-ya-kauli.html

No comments:

Post a Comment