Friday, 8 June 2012

MECHI ZA 08 JUNE 2012 - UEFA EURO 2012

19:00 Poland 1-1 Greece
21:45 Russia 4-1 Czech

NB: Saa za Afrika Mashariki.

Poland yashindwa kutamba dhidi ya Greece !
Kipindi cha kwanza kilimalizika Poland ikiongoza 1-0, kupitia bao lililofungwa na Robert Lewandowski katika dakika ya 17. Greece walikatishwa tamaa zaidi walipojikuta wakicheza pungufu baada ya Papastathopoulos kupewa kadi nyekundu. 

Kipindi cha pili kilianza vizuri kwa upande wa Greece, kwani dakika 6 baada ya kipindi kuanza walipata bao la kusawazisha kupitia Karagounis. Katika dakika ya 69 kipa wa Poland, Szczesny alipata kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Karagounis, lakini Greece walishindwa kutumia vizuri adhabu ya penalt, baada ya kipa wa Poland, kupangua. 


--------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Ni mwanzo wa safari ya mechi 31 za mashindano ya Euro 2012, wababe wa mpira wa miguu kutoka timu za taifa za nchi 16 za Ulaya watapambana. Timu hizi zimegawanywa kwenye makundi manne ya A, B ,C na D,

Mashindano haya yatadumu kwa siku siku 24, ambapo mechi ya Finali itachezwa terehe 01 July 2012, mjini Kiev (a.k.a Kyiv ) nchini Ukrain 

Leo kundi A linaaza kwa wenyeji wa mashindano haya Poland kufungua pazia dhidi ya Greece mjini Warsaw, Poland, mechi ya pili itakutanisha taifa kubwa Russia dhidi ya taifa dogo Czech.

Kesho ni kundi B: Netherlands v Denmark, Germany v Portugal 

No comments:

Post a Comment