Rais wa zamani wa Egypt, Hosni Mubarak (84), amepewa adhabu ya kifungo cha maisha jela.
Hukumu hiyo imefuatia kesi iliyokuwa inamkabili Mubarak, Habib al-Adly aliyekuwa Waziri wa zamani wa mambo ya ndani, watoto wawili Mubarak ambao ni Gamal na Alaa, wasaidizi wanne wa mubarak na mfanyabiashara mmoja.
Mubarak aliyetawala toka mwaka 1981 mpaka 2011, na wenzake walikabiliwa na tuhuma za rushwa na kushurutisha mauaji ya wanaandamanaji 850 mwanzoni mwaka 2011 waliokuwa wakipinga utawala wake, kufuatia wimbi la mabadiliko ya kisiasa lililozikumba nchi za kiarabu.
Mubarak na Habib al-Adly ndio waliokutwa na hatia kupewa kifungo cha maisha jela, wengine hawakupatikana na hatia.
Hata hivyo Gamal na Alaa awataachiwa huru sababu wanakabiliwa na kesi nyingine ya kuhujumu soko la mitaji, na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatano, 6 June2012.
No comments:
Post a Comment