Saturday, 2 June 2012

FLOYD MAYWEATHER AANZA KUTUMIKIA KIFUNGO

Bondia maarufu wa Marekani Floyd Maywether Jr (35), leo ameanza kutumikia rasmi kifungo cha siku 87 (miezi mitatu).

Mayweather alijisalimisha mahakamani huku alisindikizwa na 50 cents na mwanasheria wake, na baadaye kufungwa pingu na kuchukuliwa na askari waliompeleka Clack County Detention Centre, Nevada.

Mwezi December 2011 Mayweather alikiri mahakamani kwamba mwaka 2010 alimpiga rafiki yake wa kike wa zamani Josie Harris, na hivyo kupewa adhabu ya kifungo hicho.

Lakini Mayweather aliomba mahakama kuhairisha hukumu hiyo ili akamilishe pambano lake dhidi ya Miguel Cotto,lilifanyika 5 May 2012, ambapo Mayweather alishinda na kuendelea kushikilia ubingwa huo wa Welterweight wa WBC.

Kwenye jela hiyo yenye wafungwa 3000, Mayweather atapewa chumba cha peke yake chenye dirisha lenye kuruhusu mwanga wa jua kupita, choo, sink, kitanda na meza ya kusomea. Pia ataruhusiwa kupata magazeti mawili ama vitabu na atapewa milo mitatu kwa siku.

Akikamilisha kifungo hicho, Mayweather anatarajiwa labda atapambana na Manny Pacquaio.

No comments:

Post a Comment