Rais wa zamani wa Liberia, Charles Taylor mwenye umri wa miaka 64, amepewa adhabu ya kifungo cha miaka 50 jela.
Charles Taylor aliyekuwa anakabiliwa na mashtaka kwenye Mahakama ya Kimataifa (ICC), amepatikana na hatia ya kusaidia waasi nchini Sierra Leone, wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 1991 mpaka 2002.
Taylor anatarajiwa kukata rufaa inayotarajiwa kuanza kusikilizwa baada ya miezi 6.
No comments:
Post a Comment