Tume ya uchaguzi ya Egypt imemtangaza rasmi mgombea wa Muslim Brotherhood, Mohammed Mursi kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika.
Mohammed Mursi amemshinda Ahmed Shafiq kwa asilimia 51.73. Shafiq alikuwa Waziri Mkuu wa utawala wa Hosni Mubarak.
Ushindi huu unafungua ukurasa mpya kufuatia wimbi la mabadiliko ya kidemokrasia yaliyofanikisha kuondolewa madarakani rais wa zamani, Hosni Mubarak.
No comments:
Post a Comment