Thursday, 15 December 2011

WAZIRI MKUU WA RUSSIA AIPIGA MKWARA MAREKANI

Waziri mkuu wa Rusia, Vladmir Putin ameipiga vijembe Marekani kwa kuchochea maandamano yanayopinga matokeo ya uchaguzi wa wabunge, kwenye kipindi cha television cha maswali na majibu.

Kufuatia tuhuma zilizotolewa na Marekani (Hillary Clinton) kuhusu mapungufu yaliyojitokeza kwenye uchaguzi huo, amedai wachochezi toka nje ya Russia wanawalipa vijana ili kushiriki kwenye maandamano kupinga matokeo ya uchaguzi.

Pia amelaumu majeshi ya Marekani kuhusika na mauaji ya aliyekuwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi, kwa kushambulia (kwa ndege) msafara wake na hatimaye kwa kutumia wanajeshi (US special forces) wakawasiliana na waasi ambao walimkamata na kumuua bila kufuata taratibu za kisheria. Marekani imejibu na kusema huo ni uzushi ( ludicrous )!

Kuhusu McCain ambaye alikuwa mgombea urais wa chama cha Republican dhidi ya Barak Obama, amesema amechanganyikiwa kutokana na mateso aliyopata aliposhikwa mateka kwenye vita vya Vietnam! October baada ya Gaddafi kuuawa McCain alisema ni wakati wa madikteta kama Putin kupatwa na  woga.

Ameshauri utumiaji wa kamera kwenye vituo vya kupigia kura ili kudhibiti udanganyifu kwenye uchaguzi, amedai amefurahishwa na vijana waliondamana ikiwa ni njia ya kutoa maoni yao.

Huu ni ufa unao ongezeka kati ya Marekani na Russia, Putin akishika kiti cha urais itakuwaje!



No comments:

Post a Comment