Uenda upepo wa mabadiliko utaikimba nchi ya Zambia kufuatia uchaguzi uliofanyika jumanne !
Kulingana na tume ya uchaguzi ya Zambia (ECZ) ,matokeo yamepatikana kutoka majibo 70, kati ya hayo ni majimbo 33 yaliyothibitishwa ambapo kiongozi wa chama cha Patriotic Front (PF) ,Michael Sata anaongoza kwa silimia 46.59, raisi Rupiah Banda wa chama cha Movement for Multipary Democracy(MMD) anafuatia kwa kuwa na asilimia 33.82.
Hii ngoma ni kali kama vile mechi ya Simba na Yanga! Sababu katika uchaguzi uliopita Rupiah Banda alimshinda Michael Sata kwa kura 35000, na uchaguzi huu ni kama mechi ya marudiano, ikiwa ni mara ya nne kwa Michael Sata kugombea uraisi, waswahili wanasema mvumilivu..........!
Tume ya uchaguzi inalaumiwa kwa kuchelewesha kutoa matokeo na dalili zinaonyesha hali si shwari mitaani.
Jumla ya majimbo ni 150, na matokeo yanaonyesha dalili za chama tawala kupoteza ushindi. Je Rupiah Banda atakuwa na busara za kukubali matokeo kama akishindwa? Ama ndio mambo ya Zimbabwe kuikumba Zambia ?
No comments:
Post a Comment