Friday, 23 September 2011

MICHAEL SATA ASHINDA UCHAGUZI ZAMBIA

Michael Sata (aka King Kobra) mwenye umri wa miaka 74 ambaye  aligombea uraisi kupitia chama cha upinzani cha Patriotic Front (PF) nchini Zambia ametangazwa kuwa mshindi

Tume ya uchaguzi ya Zambia (ECZ) imetangaza kwamba Mr Sata ameshinda kwa asilimia 43% na kumzidi Rupiah Banda kwa kura 188,000. Ushindi huo umetangazwa ikiwa bado kuna majimbo 7 ayajakamilisha matokeo, kama njia ya kuepusha vurugu.

Mr Sata aliwahi kufanya kazi ya kufagia London Liverpool Station! Alikuwa Governor wa Lusaka wakati wa utawala wa Keneth Kaunda (UNIP) na alijitoa kwenye chama cha UNIP 1991 na kujiunga na MMD kilichoongozwa na Chiluba  ambapo alishika nyadhifa za uwaziri mpaka alipojiondoa mwaka 2001 na kuanzisha chama cha Patriotic Front(PF).Aligombe uraisi 2001,2006,na 2008 bila mafanikio. Pia amekuwa mtetezi wa hali bora za wafanyakazi iliyopelekea kupewa jina la King Cobra. Kuna dalili kwamba ushindi wake utatikisa mikataba mbalimbali nchini humo, pia mashirika mengi kutoka China yameshutumiwa kufadhili MMD, kama njia ya kulinda mslahi yao.

Je Rupia Banda atatoa kauli ya kukubali kushindwa? Je wawekezaji haswa kutoka China hali yao itakuwaje kwani sasa matumbo joto, kwani King Cobra ameingia madarakani!

Kama sijakosea chama cha MMD kilichukua wakati wa wimbi la maltipartism, na kuchukua madaraka kutoka wa chama cha UNIP cha Keneth Kaunda, na sasa ni PF wameingia madarakani. Zambia wamekomaa kisiasa kuliko Tanzania, kwani CCM bado ipo madarakani toka uhuru! Wakati wenzetu wamepitia vyama vingi kuongoza nchi, hivyo tunaitaji mabadiliko ili kuondoa ufisadi.




No comments:

Post a Comment