Saturday, 9 February 2013

UCHAGUZI MKUU KENYA - MDAHALO WA WAGOMBEA URAIS

Uchaguzi mkuu wa Kenya utafanyika 04 March 2013.

Wagombea sita wa urais watapambana kwenye mdahalo wa wagombea urais (presidential debate) miwili ili kujibu maswali ya mbalimbali ya wananchi.

Wagombea urais watakaoshiriki  midahalo hiyo ni Raila Odinga, Uhuru Kenyatta, Musalia Mudavadi, Martha Kirua, Peter Kenneth na James Ole Kiyiapi.

Mdahalo wa kwanza utafanyika siku ya Jumatatu, 11 February 2013, ambao utahusu maswala ya Utawala, huduma za Jamii, na mali asili. LIVE http://www.nation.co.ke/

Mdahalo wa pili utafanyika Jumatatu ya 25 February 2013. Wagombea watakumbana na maswali ya Uchumi, ardhi, madaraka na sera za mambo ya nje.

Midahalo yote itaanza saa moja na nusu usiku (19:30) kwa saa za Afrika ya Mashariki, ambapo kila mgombea atapewa dakika mbili za kujibu swali.

Zaidi ya maswali 5000 yamekusanywa kwa njia mbalimbali kupitia sms, email, twitter, facebook nk.

Midahalo hiyo itarushwa hewani kupitia radio, TV (CNN, Reuters n.k), Google (live stream) nk.

http://elections.nation.co.ke/news/All-set-for-Kenya-presidential-debate/-/1631868/1687238/-/86j9nvz/-/index.html

No comments:

Post a Comment