Tuesday 19 February 2013

MECHI ZA 19 FEB 2013 - UEFA KOMBE LA MABINGWA

22:45 Arsenal 1 - 3 Bayern Munich
22:45 FC Porto 1 - 0 Malaga

NB: Saa za Afrika ya mashariki

Arsenal inasafari ndefu, kuzidia nguvu na ujuzi wa kuchungulia goli hivi!

Bayern ilipachika bao la kwanza dk ya 7, na kuongeza la pili dk ya 21. Ndani ya dk ya 10 ya kipindi cha pili, Podolski akaipatia bao la kwanza, pamoja na Arsenal kuendeleza juhudi,lakini ni Buyern Munich waliopata bao dk 13 kabla ya kipenga cha mwisho.

Mechi ya marudiano Arsenal itatimiza wajibu tu, labda miujiza itokee.

--------------------------------------------------------------------------------------------------------
Arsenal itafuta machungu ya kutolewa kombe la FA?

Buyern Munich inaongoza ligi ya Ujerumani (Bundesliga) ikiwa na point 57, ikifuatiwa na Dortmund yenye point 42.

Arsenal ipo katika nafasi ya 5 ya ligi kuu ya Uingereza ikiwa na point 44, kwa tofauti ya point 21 dhidi ya Man Utd yenye point 65 inayoongoza ligi hiyo.

Kesho: AC Milan v Barcelona, Galatasaray v Schalke 04

No comments:

Post a Comment