Thursday 29 November 2012

UBINGWA WA FORMULA 1 MSIMU WA 2012 WAINGIA DOA , VETTEL KUVULIWA UBINGWA?

Wanasema Its not over, until........!

Brazilian Grand Prix ilifanyika 25 November na kufunga pazia la msimu wa Formula 1 kwa mwaka 2012.

Kwenye race hizo za Brazilian Grand Prix, Nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Jenson Button, wa pili Fernando Alonso na wa tatu Filipe Massa. Vettel alishika nafasi ya sita na kuibua point 8 zilizo mwezesha kufikisha point 281 na kuchukua ubingwa wa msimu wa 2012.

Hivyo Sebastian Vettel alitawazwa rasmi kama bingwa wa msimu wa 2012 baada ya kufikisha point 281, nafasi ya pili ilichukuliwa na Fernando Alonso (278) , watatu Kimi Raikkonen (207), wa nne Lewis Hamilton (190).

Lakini kuna tetesi kwamba Vettel alichakachua taratibu, hivyo kama board ya Formula 1 (FIA) utamkuta na makosa, uenda akavuliwa ubingwa hatua ambayo itamwezesha Alonso kuwa bingwa mpya ( http://www.bbc.co.uk/sport/0/formula1/20531638 )

NB: FIA imethibitisha kwamba Vettel hakufanya kosa, hivyo bado ni bingwa wa 2012

No comments:

Post a Comment