Nini kazi ya serikali na wizara husika? Chama cha siasa kinapopata madaraka, shughuli za serikali uendeshwa na wizara husika, cha kushangaza ni pale chama siasa kinapofanya kazi za wizara.

Pichani: Katibu mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana akitoa leseni kwa wachimbaji wadogo wa migodi ya Mugusi, Geita mkoani Mwanza. Kinana alikabidhi leseni 21 zilizotolewa na serekali.
Maswali:
Kinana alikabidhi leseni hizo kama nani serikalini?
Je alilipwa kufanya shughuli hiyo? Kama ni ndio, je malipo hayo yalitoka fungu lipi na kwa ruhusa ya nani?
Kama alipwi, je Wizira husika ya Madini au Biashara nk, kazi zake ni nini, na kwanini CCM ihusishwe?
Serikali na Vyama vya siasa havijui kwamba shughuli kama hiyo inakwaza wapiga kura?
Ama CCM inamiliki machimbo hayo?
Twanga link kuona zaidi: http://www.fullshangweblog.com/2012/11/23/kinana-akihutubia-maelfu-ya-watu-geita-jioni-hii/
No comments:
Post a Comment