Wednesday, 7 November 2012

OBAMA ASHINDA UCHAGUZI WA USA 2012, KUONGOZA KWA AWAMU YA PILI

Katika Uchaguzi wa USA 2012, Baraka Obama amejipatia ushindi mnono na kujihakikishia kurudi ndani ya White House kwa awamu pili ya miaka minne.

Ikiwa bado kura zinaendelea kuhesabiwa, Obama amefanikiwa kuvuka idadi ya kura (Electoral College Vote) 270 zinazohitajika, kwa kupata kura 275 dhidi ya 203 za Mitt Romney.

Romney alimpongeza Obama kwa njia ya simu kabla ya kuwahutubia wapiga kura wake na kuwashukuru.

Baada ya muda rais Obama pia alihutuba na kuwashukuru wapiga kura wa pande zote na kuahidi kushirikiana na vyama vyote.

No comments:

Post a Comment