Sunday, 18 November 2012

HAMILTON ANYAKUA USHINDI WA US GRAND PRIX

Lewis Hamilton ameibuka na ushindi wa United States Grand Prix zilizofanyika Austin, Texas na kufanya matumaini ya Sebastian Vetel ya kufungasha ushindi wa msimu kuwa ndoto.

Vetel aliyeanza katika nafasi ya kwanza alitegemewa kushinda na kukamilisha ubingwa wa msimu wa 2012 kama Fernando Alonso angemaliza chini ya nafasi ya nne. Lakini kunyume chake Vetel amemaliza katika nafasi ya pili.

Alonso aliyeanza katika nafasi ya 7 alifanikiwa kumaliza katika nafasi ya 3, na kujipa matumaini ya kupata ushindi wa msimu kwenye race za mwisho zitakazo fanyika Brazil.

Msimamo wa msimu mzima ulivyo (Top 5 ilivyo - point mabanoni) - 1.S.Vetel (273), 2.F.Alonso (260), 3.K Raikonnen (206), 4.L.Hamilton (190), 5.M Weber (167)

No comments:

Post a Comment