Saturday, 3 November 2012

HAMILTON ACHUKUA POLE KWENYE ABU DHABI GRAND PRIX, VETEL ATUPWA MKIANI

Ikiwa zimebaki race tatu za Formula 1 msimu huu, Lewis Hamilton (MacLaren) amefanikiwa kuchukua nafasi ya kwanza kwenye qualifying za Abu Dhabi Grand Prix baada ya kutumia muda wa dk 1:40.630

Bingwa wa msimu uliopita, Sebastian Vettel (Red Bull) alifanikiwa kumaliza katika nafasi ya pili kwa kutumia dk 1:40.978, lakini alishindwa kurudisha gari baada ya kupungukiwa mafuta na hivyo kupigwa adhabu ya kuanza katika nafasi ya 24 (mwisho aka mkiani) kesho.

Kufuatia adhabu aliyopewa Vettel, Mark Webber (Red Bull) aliyemaliza nafasi ya 3 ataanza katika nafasi ya 2 akifuatiwa na Maldonado katika nafasi ya 3.

Kushuwa kwa Vetel kumetoa mwanya kwa Fernando Alanso (Ferrari) kunyemelea ubingwa kama atapata point zaidi ya 13 ambayo ni tofauti ya point kati yake na Vettel. Alonso ataanza katika nafasi ya 6.

Ni nafasi nzuri kwa Hamilton kushinda point 25 kesho ingawa ni vigumu kuchukua ubingwa msimu huu. Labda ashinde race zote tatu zilizobaki ikiwemo kesho alafu Vettel na Alonso wasipate point za kutosha katika race zilizobaki.

Three races to go, nani kushinda kesho, nani atachukua ubingwa msimu huu?

No comments:

Post a Comment