Saturday 23 June 2012

WABUNGE KENYA KUHAMA VYAMA VYA SIASA BILA KUPOTEZA UBUNGE?

Nchini Kenya, uenda mbunge ataruhusiwa kuhama chama cha siasa bila kupoteza nafasi yake ya ubunge.

Jumatano, 20 June 2012, bunge la Kenya lilifanya marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa.

Mabadiliko hayo ni kumwezesha mbunge kuhama chama cha siasa bila kupoteza ubunge. Pia marekebisho ya kiwango cha elimu, ambapo mbunge lazima awe na elimu ya Chuo Kikuu (degree).

Mapendekezo ya kuhama chama bila kupoteza ubunge yalitolewa na mbunge wa Gachoka, Mh Mutava Musyimi. Baadhi ya sababu alizotaja ni idadi kubwa ya wabunge kuhama vyama vyao vya siasa, na garama ya kufanya chaguzi mpya katika maeneo husika.

Inasemekana mabadiliko hayo yatawaathiri wabunge zaidi ya 83 ambao watashindwa kutetea nafasi zao kwenye uchaguzi ujao, utakaofanyika March 2013.

Mabadiliko hayo yamepingwa na Mwenyekiti wa Tume ya katiba (Constitution Implementation Commission) Mr Charles Nyachae, baadhi ya Mawaziri, Wanaharakati na viongozi wa kidini. Wote wakishutumu ubinafsi wa wabunge hao, na ukiukwaji wa katiba.

Wanaharakati mbalimbali wanafanya juhudi za kuhitisha maandamano kupinga mabadiliko hayo na kumshinikiza Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga, kutokutia sahii mabadiliko hayo.

No comments:

Post a Comment