Wednesday, 25 April 2012

MECHI ZA 25 APRIL 2012 - UEFA LIGI YA MABINGWA

21:45 Real Madrid 3-4 Bayern Munich

NB: Saa za Afrika Mashariki

Bayern Munich waingia Fainali baada ya penalty!

Katika kipindi cha kwanza: Ronaldo aliipatia Real Madrid bao la kuongoza katika dk ya 6 kwa njia ya penalty baada ya beki wa Bayen Munich kuunawa mpira ndani ya eneo la 18. Kwenye dakika ya 13 Ronaldo akaipatia Real Madrid bao la 2. Safu ya Real Madrid nayo wakamgeuza mchezaji wa Bayern Munich kuwa sandwich ndani ya eneo la 18, Roben akapachika penalty dk ya 26 na kuwapatia Buyen Munich bao la kwanza.

Kipindi cha pili na Muda wa Ziada wa dakika 30 ulimalizika bila kupata mshindi

Hivyo dakika 120 zilimalizika Real Madrid 2 -1 Bayern , na kufanya jumla ya matokeo jumla 3-3 kwani mechi ya kwanza Bayern walishinda 2-1.

Hatimaye matuta yakapigwa, Real wakapata 1 na Bayern 3 na kufanya matokeo ya mechi hii kuwa Real 3, Bayern 4

Hongera washabiki wooote wa Bayern Munich, tuna tegemea ladha tofauti kwenye fainali.

Fainali zitachezwa : Jumanosi ya tarehe 19 May 2012, uwanja wa Allianz Arena nchini Ujerumani


-----------------------------------------------------------------------------------------------
Kama ilivyokuwa kwa Barcelona, Real Madrid walipigwa 2-1 kwenye mechi ya kwanza, na mechi hii ya marudiano inachezwa nyumbani kwa Real Madrid!

Real Madrid wanashikilia nafasi ya kwanza kwenye Ligi kuu ya Spain (La Liga), wakati Bayern Munich wapo kwenye nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga), timu hizi mbili zina hakika ya kucheza kwenye Ligi hii ya Mabingwa msimu ujao.

Bayern wanahitaji kushinda ili kuwakilisha Ujerumani kwenye fainali zitakazo fanyika nchini Ujerumani, Real Madrid watapigana kufa na kupona ili kushiriki fainali.

Fainali ni kati ya Jose Maurinho (Real Madrid) dhidi ya timu yake ya zamani (Chelsea), ama ni Bayern dhidi ya Chelsea? 

Kesho: UEFA Ligi ya Europa- Athletico Bilbao v Sporting Lisbon, Valencia v Atletico Madrid

No comments:

Post a Comment