Saturday 21 April 2012

Mh. ZITTO KABWE NA HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU

Mawaziri wazembe wanao endekeza ubinafsi wa kufuja mali na kutafuna  kodi za wavuja jasho mwisho umekaribia.

Nani angejua kwamba wabunge wanayo nguvu ya kuvunja baraza la mawaziri kama sio kupitia hoja hii ya Mh. Zitto kabwe?

Kwa mujibu wa katiba Waziri Mkuu anateuliwa na rais na Waziri Mkuu ndio mshauri wa Rais katika uteuzi wa Baraza la Mawaziri.

Mawaziri wazembe wanaweza kuwajibishwa na rais, lakini asipofanya hivyo wabunge wanaweza kumg'oa Waziri mkuu kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani naye. Hatua ambayo itasababisha kuvunjwa kwa baraza la mawaziri, ili kumpisha Waziri mkuu mpya achague baraza lake jipya la mawaziri.

Hoja ya Mh.Kabwe bado aijafikishwa kwa spika wa bunge ili ipangiwe siku ya kujadiliwa bungeni. Vikao ama msimu wa bunge unaisha Jumatatu, tarehe 23 April 2012. Na kwa maelezo ya Spika hoja inatakiwa ifikishwe siku 14 kabla ya  kujadiliwa.

Dalili zinaonyesha kwamba Spika, Anna Makinda anaelemea upande wa Serikali ya CCM badala ya kutopendelea upande wa chama chochote. Hili limejionyesha pale Mh. Makamba alipodai mwongozo kutoka kwa Spika kuhusu hoja ya Mh.Zitto, ambapo Spika alieleza kwamba hoja hiyo aina nafasi sababu bunge linamalizika kabla ya siku 14.

Uenda Spika afukui kanuni za kuendesha bunge ipasavyo. Mh.Lissu alimuomba Mh Spika mwongozo unaoruhusu kujadili hoja ambayo bado aijafika kwake, Mh Spika akajitetea kwamba hakuna kikwazo isipokuwa aitaweza kujadiliwa ndani ya vikao vya bunge hili.

Kuna dalili za kumlinda waziri mkuu kwa baadhi ya mawaziri kutaka kuachia ngazi kabla ya jumatatu, kwani wanajua kwamba waking'ang'ani madaraka kinara wao (waziri mkuu) ataenguliwa na mwishowe baraza lote mawaziri litavunjwa!

Nini kitatokea mpaka ifikapo Jumatatu?

No comments:

Post a Comment