Thursday 15 March 2012

CHAMA CHA SIASA CHA MMD NCHINI ZAMBIA CHAFUTWA

Chama Cha MMD kilitawala kwa miaka 20 kabla ya kishindwa uchaguzi wa 2011, sasa kimefutwa na msajili wa vyama nchini Zambia, kinasubiri huruma ikinusuru.

Zambia ilipata uhuru mwaka 1964 na kuongozwa na rais Keneth Kaunda wa chama cha UNIP. Mfumo wa vyama vingi ulianzishwa 1990 ambapo Chama cha MMD kiliingia madarakani tangu mwaka 1991 mpaka mwaka 2011 kupitia marais  F.Chiluba aliyeshika madaraka toka mwaka 1991 hadi 2001, Levy Mwanawasa (2002-2008), na Rupia Banda (2008-2011).

MMD inadaiwa kuwa na malimbikizo ya ada za usajili kwa baadhi ya matawi, zaidi ya Kwacha million 390 tangu mwaka 1991.

Michael Sata aliyejitoa chama cha MMD na kuanzisha chama cha Patriotic Front (PF) mwaka 2001, na hatimaye kushinda uchaguzi wa 2011, ilihaidi atambana na rushwa.

Kufuatia kufutwa chama cha  MMD uenda wabunge wake 53 wakafutiwa ubunge, jambo litakalo sababisha kufanyika kwa uchaguzi mdogo kwenye majimbo yao. Uamuzi ama huruma ya Spika wa Bunge la Zambia unasubiriwa kujua hatma ya wabunge hao.

MMD inaendelea kupata pigo kwani wiki hii mahakama nchini imebatilisha ushindi wa wabunge wawili wa MMD walioshinda uchaguzi uliopita kwenye majimbo ya Livingstone na Solwezi Mashariki.

No comments:

Post a Comment