Sunday, 25 December 2011

MAANDAMANO KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI NCHINI RUSSIA

Upepo wa mabadiliko ya democrasia unazidi kuvuma nchini Russia, kufuatia maandamano mengine yaliyofanyika kupinga matokeo ya uchaguzi wa wabunge uliofanyika 4 December 2011 ambapo chama kinacho ongozwa na waziri mkuu Vladimir Putin kilipata ushindi uliokaribia 50%

Maandamano hayo ya 24 Dec 2011 ni mwendelezo wa maandamano ya 10 Dec 2011 ambapo vyama vya upinzani vimesisitiza kwa mara nyingine kwamba matokeo ya uchaguzi wa 4 Dec 2011 yalichakachuliwa hivyo uchaguzi unastahili kurudiwa. Pia wapinzani wametoa wito kwa wapiga kura kutomchagua Waziri mkuu Putin kwenye uchaguzi wa rais utakao fanyika mwakani 4 March 2012.

Pamoja na hali ya baridi kali, waandamanaji wamekuwa ngangari na kuitikia wito wa kuudhuria maandamano hayo kwa wingi katika miji tofauti , ambapo Wizara ya mambo ya ndani imesema walioandamana katika mji wa Moscow ni watu 28,000, huku waandaaji wa maandamano hayo wamesema ni watu 120,000! (twanga link kujua zaidi - http://www.youtube.com/watch?v=nzPafnWyEX0&feature=endscreen&NR=1 )

Kwa kutumia radio station  kiongozi wa zamani wa USSR, Mikhail Gorbarchev ametoa wito kwa waziri mkuu Putin kutoshiriki uchaguzi ujao.

Katika maandamano ya 10 Dec 2011 serikali ya Russia ilishutumu mataifa na vyombo vya habari vya nje kwa kuchochea vuguvugu la maandamano nchini humo (twanga link kujua undani-   http://www.youtube.com/watch?v=4FwvQYLKK98&feature=related )

Unakumbuka wimbo 'Wind of Change' ? (twanga link- http://www.youtube.com/watch?v=Wxg_BaBvnEE&feature=related )

No comments:

Post a Comment