Sunday 13 November 2011

HATIMAYE HAMILTON ASHINDA RACE ZA ABU DHABI GRAND PRIX

Kweli mla mbivu .........!

Hatimaye Lewis Hamilton aibuka na ushindi race za Fomula 1 za Abu Dhabi Grand Prix ( Yas Marina), wakati Vetel alibaki kama mtazamaji baada tairi kupasuka sekunde chache race zilipoanza na kushindwa kuendelea ( http://www.youtube.com/watch?v=70o3d41AQZA )! Alonso alimaliza wa pili na Button nafasi ya tatu, huku Weber na Masa wakifuatia.

Tarehe 27 Novembe ni race za Brazil Grand Prix ( Interlagos) , ambazo ni za mwisho kwa msimu huu.

Nani atafunga msimu kwa ushindi, ni Vetel, ama Hamilton? Massa atakubali kushindwa akiwa nyambani! Tusubiri siku ya siku.

No comments:

Post a Comment