Saturday 29 October 2011

UGUA POLE Mh ZITTO KABWE

Hii ni habari mbaya sana, kwa mara nyingine kiongozi anapelekekwa India kwa matibabu. Serikali inabidi ichukue hatua za ziada kurekebisha hali hii ili kuokoa mateso na maisha ya watu.

Ingawa hali hii inatia shaka kwa mfumo wa huduma za afya na matibabu kwa ujumla, serikali lazima ifikiria kwanini huduma hizi hazipatikani ndani ya nchi? Sio tu nchi inatumia fedha za kigeni kutibu viongozi hawa, bali huduma hizi zikitolewa ndani ya nchi zitaokoa maisha na maumivu ya wengi kwa haraka zaidi. Pia itatoa ajira kwa wananchi haswa wataalamu nchini ambao wanataabika kutafuta kazi.

Serikali na haswa Wizara ya Afya inabidi ijiulize, kama viongozi hawa wamepelekwa nje nchini baada ya kukosa huduma ndani ya nchi, je wananchi kiasi gani wanateseka ama kupoteza maisha kutokana na mfumo huu.

Ugua pole Mh Zitto Kabwe, viongozi na wananchi wanaoteseka.

No comments:

Post a Comment