Monday 3 October 2011

IGUNGA - UCHAGUZI WA MBUNGE 2011 !

Matokeo rasmi bado ni ndoto mpaka muda huu!

Pamoja na majigambo ya tume ya Uchaguzi kwamba walijiandaa vizuri na kudai kwamba matokeo yatatoka ndani ya masaa 24, lakini ahadi hizo zinaelekea kuyeyuka.

Kama mwendo huu utaendelea uenda hali isiwe shwari kwani subira kwa baadhi ya wapiga kura inaanza kutoweka na mabomu ya machozi yameanza kutumika ili kutawanya baadhi ya wananchi wanaodai matokeo. Baadhi ya shughuli haswa za kibiashara zimesimama. 

Uenda matokeo rasmi yatatoka muda wowote na mchuano ni mkali kati ya CCM na CHADEMA, je hali itakuwaje? Chama kitakachoshindwa kitakubali kushindwa ? Je kutakuwepo uchakachuaji matokeo? Nini tathmini ya ufanisi katika shughuli nzima za uchaguzi?

Tuvute subira.

No comments:

Post a Comment