Saturday 1 October 2011

UCHAGUZI MDOGO IGUNGA- SASA KUMEKUCHA

Hayawi hayawi ..........!  Asiye na mwana aelekee jiwe!

Wala sio uchaguzi mkuu, bali ni uchaguzi mdogo kufuatia kujiuzulu aliyekuwa mbunge, Ndugu Rostam Azizi. Hatimaye kama desturi imebidi ufanyike uchaguzi kumpata mbunge atakayewakilisha wilaya ya igunga. Yamezuka mengi utadhani uchaguzi wa raisi, huku chama tawala kikitumia kila nama kuhakikisha kinapata ushindi , na vyama pinzani vikitunishasha misuli kuashiria kwamba huu ni wakati wa mabadiliko.

Baadhi ya matukio yaliyojitokeza:-
-Mwenyekiti wa wazee wa chama cha CUF kulazwa baada ya kipigo alichopata kutoka kwa vijana wa CCM.
-Kijana kumwagiwa tindikali, inasemekana ni baada ya kuwageuka vijana  wenzake wa CCM waliokuwa kwenye harakati za kuujumu harakati za CHADEMA.

-Katibu wa CCM, Mukama aliishutumu CHADEMA kuingiza magaidi waliopata mafunzo Uarabuni, huku mbunge wa CHADEMA Mh Lisu akipinga vikali tuhuma hizo.

-Mkuu wa wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario kukamatwa na vijana wa CHADEMA na kufikishwa kituo cha pilice,baada ya kukutwa akiendesha mkutano kinyume na taratibu, swala hili lilizua mzozo  kwamba alivuliwa hijabu kinyume na taratibu za kidini na kwamba ni udhalilishaji. Swala hili bado linauchunguzwa na police.

-Balozi wa mtaa fulani, mzee Maboko Masele (CCM) alikutwa na daftari lenye list ya wapigakura, alidaiwa katika harakati za kuchakachua majina ya wapiga kura, mzee huyo baada ya kubanwa alisema ni agizo lililotolewa kwa mabalozi wote. Nia ilikuwa nini, jibu hakuna mapaka sasa.

-Silaha ilitumika katika kile kilichodaiwa ni harakati za kumuokoa mbunge Esther Bulaya(CCM) kufuatia njama za CHADEMA kutaka kumteka, ambapo ndugu Waitara (CHADEMA) alihusishwa. swala hili linachunguzwa na police.

-Mbunge Aden Rage alihuhutubia kwenye mkutano , huku silaha yake ikionekana wazi kiunoni ikiwa ni kinyume na taratibu.

-CHADEMA ilituhumu CCM kuingiza mabox na karatasi bandia za kupigia kura.

-CHADEMA iligundua mpango wa CCM wa kwaandaa watu watakaovyalishwa magwanda ya CHADEMA kisha wachome majengo mawili ya CCM, ili baadae wadai kuwa wametumwa na CHADEMA, ikiwa ni njia ya kuwachafua.

-Vijana wa CCM wakisaidiwa na Mh Makamba waweka kizuizi barabarani na kusimamisha mabasi yanayodaiwa kubeba vijana wa CHADEMA wanaotoka nje ya wilaya ya Igunga wakiwa na silaha kwenda kufanya fujo Igunga, ingawa katika upekuzi silaha azikupatikana.

Hayo na mengine mengi yamezuka, huku Msajili wa Vyama vya siasa akiilaumu Tume ya Uchaguzi (NEC) kutowajibika katika kuthibiti ukiukwaji wa taratibu unaofanywa na vyama na wagombea.

Nayo NEC imedai kufanya kila jitihada kuepusha vurugu na ukiukwaji wa taratibu, ikiwa na pamoja na kuvitaka vyama vya siasa kukutana na kuondoa tofauti zao, jambo ambalo lilifanyika. Pia NEC ilidai kwamba maswala mengine yapo mikononi mwa police na hivo si rahisi kuyaingilia.

Pamoja matukio yote hayo, sasa wakati umefika tarehe 2 Oct 2011 (kesho) ni siku ya kupiga kura na NEC imedai kujiandaa vyema kuhakikisha matokeo yanatoka baada ya masaa 24, naamini itakuwa Jumatatu jioni ama mapema Jumanne.

Idadi ya wapiga kura-174077;  Vituo vya kupiga kura-427. Vyama vikuu ni CCM , CHADEMA, CUF ambapo mshindi lazima atoke!

Ilikuwa safari ndefu, vyama pinzani CUF, CHADEMA nk vimejitahidi sana. Nani ataibuka mshindi?  Je nini kitafuata baada ya matokeo, ama ni yale mambo ya kupelekana mahakamani kupinga matokea? Tusubiri matokeo, macho na masikio tuyaelekeze Igunga.

No comments:

Post a Comment