Wednesday 31 August 2011

TANZANIA ITOE TAMKO KUHUSU WAASI (NTC) LIBYA

Serikali ya Tanzania inabidi kutoa msimamo kuhusu waasi nchini Libya.

Kuunga mkono waasi walioiangusha serikali ya Gaddafi si jambo la kujadili kwa sasa, kwani Tanzania ni mwanachama wa United Nations (UN),  na Mtanzania Asha Rose-Migiro ni naibu katibu mkuu wa umoja huo ambao ulipinga ukandamizaji uliofanywa na uongozi wa Gaddafi. Uamuzi wa kuruhusu majeshi ya NATO kutumika kuzuia mauaji ya wananchi wa Libya ni sababu tosha isiyohitaji mjadala kwani mafanikio yamepatikana na serikali ya Tanzania inapaswa kuwakubali waasi bila kusita.

Serikali ya Tanzania lazima ionyeshe mfano kwa mataifa mengine kwamba unyanyasaji wa raia unaofanywa na baadhi ya viongozi wa Afrika sio sahihi, kama ilivokuwa Uganda enzi za Iddi Amin. Tanzania ilionyesha msimamo wake kwa kumwondoa Amin madarakani kwenye vita vya Kagera na pia Tanzania ilisaidia nchi nyingi kupambana na ukandamizaji kama vile Msumbiji , Afrika ya kusini nk.

Pia Tanzania imejipatia sifa nzuri barani Afrika na diniani  kwa kukubali mahakama ya ICTR (International Criminal Tribunal for Rwanda) kuweka shughuli zake mjini Arusha kushughulikia mauaji ya Rwanda.

Kwanini serikali inasita kutoa tamko? Ama kuna agenda ya siri! Vingozi wengi wa Afrika walipata misaada ya kila aina ikiwemo ya kifedha toka kwa Gaddafi. Inawezekana hata  vyama vingi tawala barani Afrika vimewezeshwa kuwepo madarakani kutokana na misaada ya Gaddafi. Labda Gaddafi alitumia nafasi yake na utajiri wa Libya kutekeleza ndoto zake ikiwa ni kuundwa kwa Umoja wa Afrika (United State of Africa) hapo baadae, lakini alisahau kwamba wananchi wa Libya wanahitaji uhuru wa kweli.

Serikali ya Tanzania inabidi kuwajali wananchi wa Libya na sio vinginevyo, bila kujali msimamo wa AU (Africa Union). Hivyo kauli ya kuwakubali waasi ni muhimu.

No comments:

Post a Comment