Monday 29 August 2011

LIBYA- GADDAFI BADO MAFICHONI

Wiki moja sasa tangu waasi (NTC) wameingia mji wa Tripol na kuumiliki. Na sasa nguvu zote zimeelekezwa mji Sirte alikozaliwa Gaddafi.

Ndani ya wiki hiyo yamefichuliwa mengi ikiwemo jela za wafungwa waliokuwa wakipinga utawala wa Gaddafi, hazina ya silaha alizokuwa anatumia Gaddafi, na jinsi gani Gaddafi na familia yake walivokuwa wananaishi maisha ya kifahari kwa kutumia mali za nchi hiyo. Pia kuna tetesi kwamba mtoto wa Gaddafi aliyeuwawa na majeshi ya US, Hanna Gaddafi uenda yupo hai, kwani baadhi ya report za shule ama chuo alichosoma hivi karibuni  zilipatikana, ingawa inahisiwa uenda jina hilo alipewa ndugu mwingine kama kumbukumbu ya Hanna.

Waasi (NTC ) wameendelea kukubalika na jumuiya za kimataifa ikiwepo umoja wa nchi za ulaya (EU) , nchi za Kiharabu nk. Cha kushangaza ni viongozi wa Afrika (AU) ambao ndio wangekuwa mstari wa mbele kujali maslahi ya wananchi wa Libya badala yake wanausasua sababu viongozi wengi wa Afrika wapo madarakani kimabavu kama Gaddafi , na pia misaada mingi iliyotolewa na Gaddafi iliwawezesha viongozi wengine wa Afrika kuwa madarakani.

Katika kipindi cha wiki moja Gaddafi ameanza kupungua nguvu na ametoa wito kupitia msemaji wake mkuu Moussa Ibrahim kwamba anataka mazungumzo ili kukabidi madaraka kwa NTC. Ingawa waasi wamekataa  mazungumzo kwani kazi imefika mwisho .

Tanzania inashangaza , kwanini serikali aijatoa tamko la kuikubali NTC mpaka leo? Mbona Tanzania ilisaidia Uganda  kumg'oa Idd Amin madarakani? Pia Tanzania ni makao makuu ya mahakama ya kimataifa (ICTR) iliyoko mjini Arusha inayo shughulikia mauaji ya Rwanda, mahakama hiyo imeipa sifa mji wa Arusha kama Geneva of Afrika ambayo ni makao makuu ya mahakama hiyo. Majeshi ya Gaddafi yamefanya mauaji ya raia wengi wasio na hatia yanayofanana na yale ya Uganda na Rwanda.

Waasi (NTC) watafanikiwa kuyaondoa majeshi ya Gaddafi katika mji wa Sirte lini? Labda siku kama ya leo wiki ijayo watafanikisha. Yapi yatafichuliwa zaidi kuhusu Gaddafi, na Gaddafi atajisalimisha lini?








No comments:

Post a Comment