Thursday 11 August 2011

MAHAKAMA UK IMERUHUSU MTUHUMIWA KUPELEKWA S/AFRICA

Judge wa mahakama nchini UK ameruhusu mtuhumiwa aliyehusishwa na kifo cha mke wake kupelekwa Afrika Kusini kusomewa mashitaka. Maamuzi ya mwisho yanategemewa kutolewa na Waziri wa mambo ya ndani.

Mtuhumiwa huyo Shrien Diwani alikwenda SA kwa honeymoon baada ya ndoa yao, lakini baada ya siku chache wakiwa South Africa(SA) mke wake aliuawa baada ya gari (taxi) kuvamiwa na mke wake kuuliwa na majambazi hao.

Dereva wa taxi hiyo alidai kuwa Shrien aliwalipa ili kutekeleza mauaji hayo. Ni muda mrefu mtuhumiwa huyo amekuwa akitoa sababu mbalimbali ikiwemo magonjwa nk. zilizochelewesha maamuzi ya mahakama nchini UK kutolewa kuhusu kuruhusu kwa mtuhumiwa huyo kupelekwa SA kusomewa mashitaka , ambapo mahakama ya nchini SA imedai kunavithibitisho kwamba alihusika na anastahili kupelekwa kusomewa mashitaka.

Uamuzi wa warizi wa mambo ya ndani unasubiriwa kujua hatima ya mtuhumiwa.

for more- http://www.bbc.co.uk/news/uk-england-14477461

              - http://www.bbc.co.uk/news/uk-england-bristol-11937170

No comments:

Post a Comment