Tunachosikia ni viongozi wa serikali ya CCM inavyohimiza wananchi kuhusu sherehe za miaka 50 ya uhuru,.
Inabidi tujiulize nini mafanikio na mapungufu yaliyojitokeza kwa muda wote huo wa miaka 50?
Je wananchi tunaelewa chochote, ama tunaburuzwa na propaganda za itikadi za kisiasa ili kutimiza matakwa ya viongozi waliopo madarakani, bila kujali uelewa wa wananchi wa hali ya chini?
Je tofauti kati ya masikini na matajiri imepungua ama imeongezeka? Je huduma za Elimu, Afya, usafiri zipo katika hali gani tukilinganisha na wakati tunapata uhuru , na nchi jirani na dunia kwa ujumla.
Je tatizo la umeme, ndio kipimo kikubwa cha mafanikio ya nchi, tukijua kwamba shughuli nyingi zinategemea umeme kwa maendeleo ya nchi, na ahadi za kutatua tatizo la umeme zimekuwepo tangu lini, na mafanikio gani yamefikiwa?
Je nchi ya Tanganyika ipo kwenye nafasi gani katika sherehe hizi ama ni kiini macho?
Tujiulize tunasherehekea miaka 50 ya umasikini ama mafanikio? na nani apongezwe ama awajibike?
No comments:
Post a Comment