Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema (CHADEMA) afikishwa kwenye Mahakama ya Mkoa wa Arusha na kushitakiwa kwa makosa ya uchochezi.
Uchochezi huo unahusishwa na maandamano yaliyopangwa na wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), kufuatia kifo cha mwanafunzi mwenzao.
Moja ya kosa linalo mkabili Mh Lema ni kuwaambia wanafunzi wa hao kwamba 'Kosa kubwa kuliko zote duniani ni woga', ujumbe pichani juu.
Pichani juu: Kushoto Mh Lema kizimbani akisomewa mashtaka, kulia wafuasi wa CHADEMA wakiwasindikiza kamanda Lema na Mh Nasari juu ya gari.
Pichani wapenzi wa CHADEMA wakitoa ujumbe kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, aliyetoa amri ya kukamatwa kwa Mh Lema. Kuona mapicha lukuki twanga link - www.jamiiblog.co.tz
Kesi inayo mkabili Mh Lema inatarajiwa kuendelea siku ya Jumatano, 29 May 2013.
CHADEMA inatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara mjini Arusha siku ya Alhamisi wiki hii.
No comments:
Post a Comment