Monday, 4 March 2013

UCHAGUZI MKUU KENYA 04 MARCH 2013, NANI KIUBUKA NA USHINDI

04 march 2013 ni siku ya uchaguzi mkuu nchini Kenya ambapo upigaji kura umeanza saa 12 asubihi na unatarajiwa kumalizika saa 11 jioni.

Mshindi wa nafasi rais anatakiwa kupata zaidi ya nusu ya kura zote na angalau robo ya kura kwenye counties (wilaya) 24 kati ya 47, la sivyo wagombea wawili watakaopata kura nyingi watapambanishwa kwenye uchaguzi mwingine ili kupata mshindi.

Kuna wagombea nane wa urais, na mchuano mkubwa ni kati ya Raila Odinga wa Cord na Uhuru Kenyatta wa Jubillee Alliance. Hata hivyo Odinga anapewa nafasi kubwa ya ushindi.

Ijumaa, 01 march 2013 ilikuwa siku ya mwisho wa kampeni, Bw Odinga alisisitiza kwamba anataka ushindi upatikane ndani ya dk 90 na sio kwenye muda wa nyongeza, akiwahimiza wapiga kura wake kupata ushindi ifikapo saa 3 asubuhi.

Kwa upande mwingine, Uhuru alimkumbusha Odinga kukubali kushindwa baada ya matokeo.

Nani ataibuka na ushindi na kuwa rais wa 4?

Kufuatilia live twanga link...  http://www.nation.co.ke/ , au http://www.standardmedia.co.ke/ktn/live

No comments:

Post a Comment