Sunday, 23 September 2012

MECHI ZA 23 SEPT 2012 - LIGI KUU YA UINGEREZA

15:30 Liverpool 1-2 Manchester Utd
17:00 Newcastle Utd 1-0 Norwich City
18:00 Manchester City 1-1 Arsenal
18:00 Tottenham 2-1 QPR

NB: Saa za Afrika Mashariki

Bwawa la maini laendelea kukauka, Man City yavutwa shati!

Gerald aliipatia Liverpool bao la kuongoza dk ya kwanza ya kipindi cha pili, lakini baada ya dakika 5 Rafael akaisawazishia Man Utd,  na dakika 9 kabla ya mchezo kumalizika Van Parsie akaipatia Man Utd bao la pili kwa njia ya penalty.

Man City nayo ilifanikiwa kuchungulia lango la Arsenal dk 5 kabla ya mapumziko kupitia Lescot. Huku Arsenal ikionyesha mchezo mzuri kuliko mabingwa watetezi ilifanikiwa bao la kuzawazisha dk ya 77 bao lililofungwa na Koscielny.

Top 7 ilivyo baada ya mechi (point mabanoni): 1.Chelsea (13), 2.Man Utd (12), 3.Everton (10), 4. West Bromwich (10), 5.Arsenal (9), 6.Fulham (9), 7.Man City (9) 

Mechi nyingine ya kukata na shoka Jumamosi ijayo ni ya Arsenal v Chelsea
   
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------
Kabla ya mechi:
Man Utd inashikilia nafasi ya 5 ikiwa na point 9, ushindi utaisogeza mpaka nafasi ya 2 ama ya 3 kulingana na matokeo ya Man City v Arsenal! Bwawa la maini (Liverpool) ipo nafasi ya 18 inazo point 2, inawezekana wakasafisha nyota (kupata ushindi) kupitia Mashetwani Wekundu?

Man City ipo nafasi ya 7, Arsenal nafasi ya 6  na zote zina point 8. Arsenal ikipata matokeo ya sare ugenini si mbaya, ushindi nao ni ahhh..! Mabingwa watetezi watakubali kupoteza uwanja wa nyumbani?

No comments:

Post a Comment