Wednesday, 1 August 2012

SAFARI YA TEAM TANZANIA KWENYE LONDON OLYIMPIC 2012

Team Tanzania  kwenye mashindano ya London Olympic 2012 inayo mtihani mgumu, kwani washiriki watatu kati ya 7 wameshatolewa kwenye mashindano.


Pichani mbele toka kushoto: wa pili ni Magdalena Moshi na watatu ni Ammaar Ghadiyali

Kwa upande wa masumbwi, Suleimani Kadunda alitolewa 29 July 2012, baada ya kushindwa kwenye pambano la welter (69kg) dhidi ya B Vasilii wa Moldova.

Kwenye mashindano ya kuogelea ya 100m freestyle yaliyofanyika 31 July 2012 kwa upande wa wanaume, mshiriki wa Tanzania, Ammaar Ghadiyali (15) alitolewa kwenye mchujo wa kwanza (heats) baada ya kutumua muda wa dk 1.07.01, na kushika nafasi ya 55 kati ya washiriki 56. Aliyeongoza ni mshiriki wa Marekani aliyetumia muda wa sekunde 48:19.

Pia kwenye mashindano ya kuogelea 100m freestyle kwa wanawake yaliyofanyika 01 August 2012 (leo), mshiriki wa Tanzania, Magdalena Moshi ametolewa kwenye mchujo wa kwanza (heats) baada ya kutumia muda wa dk 1.05.80 na kushika nafasi ya 45 kati ya washiriki 48. Aliyeongoza ni mshiriki wa China aliyetumia muda wa sukunde 53.28.

Waliobaki ni wanariadha watakaoshiriki kama ifuatavyo:

07 Aug: Wanawake 5000m - Zakia Mrisho

12 Aug: Wanaume marathon - Mohamedi Msandeki, Faustine Mussa, na Samson Ramadhani

No comments:

Post a Comment