Waziri wa Usalama wa ndani ya nchi (Internal Security) wa Kenya, Prof George Saitoti na naibu wake, Mh.Joshua Orwa Ojede, wamefariki dunia kufuatia ajali ya ndege aina ya Eurocopter.
Ajali hiyo imetokea eneo la Kibuku, Ngong, ambapo pia walinzi wawili na pilot wawili wamepoteza maisha.
Waziri huyo na naibu wake walikuwa wakielekea wilaya ya Ndiwa iliyopo jimbo la Nyanza Kusini, ambalo ni jimbo la Mh Ojede, kwa ajili ya harambee ya Kanisa Katoliki la Nyarongi.
Pamoja na vitu vingine, mabaki ya fedha (noti) kwa ajili ya harambee hiyo yalikuwa yamezagaa eneo la ajali.
Saitoti alikuwa akitarajiwa kugombea urais kwenye uchaguzi ujao wa mwaka 2013.
Serikali ya kenya imetangaza siku tatu za maombolezo kitaifa kuanzia jumatatu, ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti.
No comments:
Post a Comment