Wednesday, 30 May 2012

MWANZILISHI WA MTANDAO WA WIKILEAK APOTEZA RUFAA

Mwanzilishi wa mtandao wa WikiLeak, Julian Assange (40) amepoteza rufaa katika mahakama kuu nchini Uingereza.

Asange ambaye ni mzaliwa wa Australia, kwa sasa anaishi nchini Uingereza, anahitajika nchini Sweden kujibu tuhuma za kujamiiana na mwamamke bila ya idhini yake mwaka 2010.

Asange amepinga madai hayo na kudai kwamba ni njama za kumfunga mdomo kutokana na kufichua maovu ya makampuni na serikali mbalimbali duniani, ikiwemo Marekani na pia Tanzania

Hata hivyo kesi hiyo inatarajiwa kurudiwa ndani ya siku 14, baada ya kugundulika kwamba kigezo kilichotumika kutoa uamuzi, akikupewa nafasi ya kujadiliwa na upande wa utetezi.

No comments:

Post a Comment