Wanasema kelele za chura.......................................!
Kama ulinukuu majigambo ya Carl Froch kabla ya mpambano (angalia -MASUMBWI - FROCH v WARD), nadhani uligundua kwamba ameshinda! Lakini kipigo alichopokea (twanga link- http://www.youtube.com/watch?v=bjWVNTmKXxA ) Froch amekiri mwenyewe kwamba hakuwa uwezo wowote wa kufurukuta dhidi ya Ward.
'Ward anaweza kupigana akiwa katikati na pembeni ya ulingo, pia akiwa uso kwa uso anaweza kurusha makonde ya uhakika kwenye kichwa na kwenye mwili, masumbwi yake ni ya kasi kubwa (speed) na anajua kuwepa, hivyo sikujua lakufanya (I couldn't really get anything going, he was too slippery)' hayo ni baadhi ya maneno ya Froch!
Sio tu Froch hakupata ushindi wa Super Six Champions, bali amepoteza mkanda wa WBC (Super Middleweight) aliokuwa akishikilia kwa muda mrefu, na kufuata nyayo za Mwingireza mwenzanke Amir Khan ambaye alipoteza mikanda yake miwili dhidi ya mmarekani Peterson (angalia -http://tanganyika2day.blogspot.com/2011/12/masumbwi-amir-khan-apigwa-na-lamont.html)
Froch mwenye umri wa miaka 34 anacho kilima kikubwa kurudisha hadhi yake kama sio kukaribia kustaafu, huku Ward mwenye umri wa miaka 27 ndio kwanza kumekucha anashikilia mataji ya Super Middleweight: WBA na WBC na Super Six Champions, baada ya kushinda kwa point 118-110 ,115-113
Nani atajitokeza kumpa Ward ushindani? Anamaliza mwaka kwa furaha isiyokifani.
No comments:
Post a Comment